HII NDIO MAANA HALISI YA WIKI KUU KWA WAKRISTO WAKATOLIKI
HII NDIO MAANA HALISI YA WIKI KUU KWA WAKRISTO WAKATOLIKI
WA AMBAO HAWAJUI RATIBA YA WIKI HII KUU YA MATESO YA BWANA WETU YESU KRISTO KATIKA LITRUJIA YA KANISA, IKO KAMA IFUATAVYO:-
1. JUMATATU KUU
Hii ni siku maalumu ambayo Yuda anajitoa mwenyewe kabisa katika Jumuiya ya Mitume, na kuanza mipango yake kabambe ya kumuuza Yesu.
2. JUMANNE KUU
Hii ndiyo siku ambayo Yuda anatimiza mipango yake ya kumsaliti Yesu na kukabidhiwa vipande thelathini (30) vya fedha.
3. JUMATANO KUU
Hii ndiyo siku ambayo Yesu anawajulisha na kuwatangazia Mitume wake juu ya mpango wa Yuda, japo kwa mafumbo na kueleza waziwazi yale yatakayompata.
4. ALHAMISI KUU
Hii ndiyo siku ambayo, wakati wa jioni Yesu anaweka sakramenti kuu mbili ambazo ni: EKARISTI TAKATIFU na DARAJA TAKATIFU pamoja na AMRI KUU YA MAPENDO.
5. IJUMAA KUU
Hii ndiyo siku ambayo, asubuhi na mapema (Alfajiri) Yuda anapokea kikosi cha maaskari tayari kwa kumsaliti Bwana wake, Mwalimu na Muumba wake.
Hapa naomba niseme kidogo, kwa utamaduni wa Waisraeli kulikuwa na salamu za mabusu za aina tatu (3) ambazo ni:
1. Salamu ya Bwana na Mtumwa - ambapo mtumwa alitakiwa kulala kifudifudi na kubusu miguu ya Bwana wake.
2. Salamu ya Mwalimu na Mwanafunzi wake - ambapo mwanafuzi alipaswa kupiga goti moja na kubusu mkono au mikono ya Mwalimu wake. Na hii ndiyo salamu ambayo Yuda alipaswa kumsalimia Bwana Yesu siku zote hata pale bustanini Gethsemane. Kwani hata Watumishi wa Altare hufanya hivi pale wanapokutana na Mapadre au wakati wa kutoa amani.
3. Salamu ya Mwalimu kwa Mwalimu, Bwana kwa Bwana, Wakuu kwa Wakuu - Mara nyingi hawa husalimiana kwa kubusiana mashavu wakiwa wamesimama.
Mpaka hapo mtakuwa mmelewa jinsi usaliti wa Yuda ulivyokuwa mkubwa, na nini maana ya swali la Yesu kwa Yuda aliposema: " Yuda unamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
Pia siku hiyo hiyo ya IJUMAA KUU, Yesu anahukumiwa afe majira ya saa 3:00 asubuhi, saa 6:00 mchana anasulubiwa, saa 9:00 alasiri anakufa pale Msalabani na saa 12:00 jioni anazikwa ili kupisha Sabato iingie.
Comments
Post a Comment