Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.02.2020: Skriniar, Tah, Alonso, Klopp, Hodgson, Lallana

Haki miliki ya pichaAFP
Image
Jurgen KloppHaki miliki ya pichaAFP









Image caption
Wachezaji wa Atletico wanamtaka Jurgen Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa.

Wachezaji wa Atletico Madrid walishikwa na hasira na kushangazwa baada ya kukosolewa na kocha wa Liverpool Jurgen Klopp. Atletico iliwafunga Liverpool 1-0 Jumanne katika raundi ya kwanza ya hatua ya mtoano ya Kombe la Mabingwa Ulaya, wachezaji wa Atletico wanamtaka Klopp kutizama mapungufu ya timu yake badala ya kuwakosoa. (ESPN)

Manchester City na Barcelona wanaminyana kumsajili beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, na klabu itakayofanikiwa kumnyakua itabidi itoe dau la zaidi ya pauni milioni 75. (Calciomercato)

Arsenal wanapanga kumsajili beki wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah ambaye kwa mujibu wa mkataba wake anathamani ya pauni milioni 34. (Bild - in German)

Jonathan TahHaki miliki ya pichaTF-IMAGES
Image captionJonathan Tah

Beki wa pembeni wa Chelsea Marcos Alonso, 29, bado yungali anawaniwa na Inter Milan lakini klabu yake inatarajiwa kuongeza bei ya mauzo ya mchezaji huyo. (Calicomercato - in Italian)

Mwenyekiti wa Crystal Palace Steve Parish anaamini wataendelea kusalia na kocha Roy Hodgson baada ya kumpatia mkataba mpya. (Sky Sports)

WillianHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkataba wa Chelsea na Willian kufikia kikomo mwishoi mwa msimu.

Winga wa Brazil Willian, 31, ambaye mkataba wake na Chelsea unamalizika mwishoni mwa msimu anasema hana mpango wa kuihamisha familia yake kutoka kwenye nyumba yao jijini London. (Mail)

Klabu ya Inter Milan inajipanga kutoa wachezaji kwenda klabu ya Verona kama sehemu ya mpango wa kumnasa beki wa Albania Marash Kumbulla, 20, ambaye pia anawaniwa na Liverpool. (Inside Futbol)

Marash KumbullaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarash Kumbulla anawaniwa na Inter Milan na Liverpool

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer alikuwa akitaka kumsajili kiungo Christian Eriksen, 28, kabla raia huyo wa Denmark kuhamia Inter Milan akitokea Tottenham. (Manchester Evening News)

Klabu za Juventus na Inter Milan wanavutiwa kumsajili beki wa pembeni wa Chelsea Emerson Palmieri, 25, lakini bado ofa rasmi hazijatumwa ajenti wake abainisha. (Goal.com)

David LuizHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionDavid Luiz alishinda Kombe la Europa msimu uliopita na Chelsea, anaamini msimu huu atashinda tena na Arsenal.

Beki wa Brazil David Luiz, 32, anaamini Arsenal wana kiwango cha ubora cha kuwafanya washinde Ligi ya Europa msimu huu baada ya kushindwa msimu uliopita.(Evening Standard)

Klabu ya Real Madrid wanamfuatilia kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Marca)


Comments

Popular posts from this blog

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

Differences between Gymnosperms and Pteridophytes

Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke