David Obola mbunge mmoja wa Uganda aliyebeba nzige na kupeleka bungeni habari kamili hii hapa
Video ya mbunge mmoja wa Uganda aliyebeba na kupeleka nzige bungeni imesambazwa katika mitandao ya kijamii.
David Obala ambaye anaiwakilisha kaunti ya Ngora Mashariki mwa Uganda , aliwapeleka nzige hao bungeni siku ya Jumanne ili kupinga hatua ya serikali ya kuchelewa kuliangazia janga la kukabiliana na mlipuko wa wadudu hao ambao wameharibu mimea katika eneo la Afrika mashariki hatua inayozua hofu ya kusababisha baa la njaa.
Baada ya mbunge mwIngine kulalamika, bwana Obala alilazimika kuikabidhi chupa iliojaa nzige kwa afisa wa bunge anayesaidia katika kuweka amani bungeni.
Spika alitaka kuelezewa kila wiki kutoka kwa wizara kuhusu hatua ya serikali ya kuwanyunyuzia dawa wadudu hao.
Gazeti la Daily Monitor nchini Uganda lilituma ujumbe wa twitter wa video hiyo ambapo mbunge huyo alionekana akiwabeba nzige hao.

Comments
Post a Comment