Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.10.2019

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 22.10.2019: Pochettino, Ferguson, Giroud, Eriksen, Abraham, Fred


Mauricio PochettinoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKocha wa Tottenham,Mauricio Pochettino(katikati)
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino, anasema kuwa anahofia kufutwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo (Mirror)
Juventus na Atletico Madrid zinamfuatilia beki wa West Brom wa miaka 19, Nathan Ferguson.(Sun)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33, anatakiwa na Crystal Palace na huenda akajiunga na klabu hiyo ifikapo mwezi Januari. (Daily Star)
Olivier GiroudHaki miliki ya pichaAFP
Image captionOlivier Giroud
Real Madrid haitajaribu kumsaini mchezaji wa safu ya kati wa Tottenham raia wa Denmark, Christian Eriksen, 27, mwezi Januari hadi watakapowauza wachezaji wasiokuwa katika kikosi cha kwanza. (AS)
Real itaipatia Spurs kiungo wao wa kati wa Uhispania Isco, 27, na mshambuliaji wa Jamuhuri ya Dominica Mariano Diaz, 26, katika juhudi ya kupata saini ya Eriksen. (El Desmarque - in Spanish)
Mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham, 22, anakaribia kutia saini mkataba mpya wa kusalia Stamford Bridge baada ya kufunga mabao manane katika ligi ya Premia msimu huu. (Daily Star)
IscoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsco, Kiungo wa kati wa Real Madrid
Barcelona imemaliza mzozo wake na Atletico Madrid kuhusu usajili wa Antoine Griezmann, 28, kwa kumlipia euro milioni 15 zaidi mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (El Mundo - in Spanish)
Derby itampatia nahodha wa zamani wa England Wayne Rooney, 33, mafunzo maalum kuhakikisha yuko tayari kwa mashindano atakapojiunga na klabu hiyo kutoka DC United. (Mail)
Kiungo wa kati wa Brazil na Manchester United Fred, 26 - ambaye alinunuliwa kwa kima cha £47m kutoka Shakhtar Donetsk mwezi Juni 2018 - anaamini kuwa ameanza kupata uzoefu wa soka la Uingereza. (Telegraph)
Antoine GriezmannHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAntoine Griezmann
Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa RB Leipzig na Ufaransa wa chini ya miaka-21 Dayot Upamecano, 20, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 50. (Mail)
Meneja wa Italia Roberto Mancini huenda akamjumuisha kipa mkongwe wa Juventus Gianluigi Buffon, 41, na kiungo wa kati wa Boca Juniors wa miaka 36 Daniele de Rossi katika kikosi cha Euro 2020. (Rai Sport via Mail)
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema anataka kusalia klabu hiyo maisha. (Marca)
Zinedine ZidaneHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane
Beki wa zamani wa Arsenal na England Sol Campbell, 45, anafanya mazungumzo ya kuwa mkufunzi wa Southend, inayoshiriki soka la daraja ya kwanza - miezi miwili baada ya Macclesfield inayocheza soka ya daraja la pili. (Sun)


                              @ Follow on Instagram
r_dj_lyimo 

Comments

Popular posts from this blog

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

Differences between Gymnosperms and Pteridophytes

Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke