Wafanyakazi Afrika Mashariki waambulia patupu
COTU
Wafanyakazi wa Afrika Mashariki hawana sababu ya kutabasamu, baada ya serikali zao kuwanyima nyongeza ya mishahara, wakati wa sherehe za kuadhimisha siku kuu ya wafanyakazi duniani
Nchini Kenya licha ya wafanyakazi kuwa wachangamfu na wenye furaha, tangazo walilosisubiri silo walilosikia.
Waziri wa leba (kazi) nchini Kenya Ukur Yattani amesema kuwa suala hilo lingali linajadilkiwa na washika dau, hali iliyowafanya wafanyakazi waliokuwa wakihudhuria sherehe hizo mjini Nairobi kuondoka wakati waziri alipokuwa akitoa hotuba hiyo ya rais.
Badala yake sherehe za siku ya wafanyakazi zilitawaliwa na miito kutoka kwa wanasiasa ambao wameilaumu serikali kwa kujaribu kuongeza mzigo kwa wafanyakazi kwa kuwatoza ushuru zaidi ili kugharamia ujenzi wa nyumba za bei ya chini.
- Semenya ashindwa rufaa dhidi ya sheria za IAAF
- Tanzania haitaongeza muda wa likizo ya uzazi
- Picha bora za chakula
- 'Liverpool itapata tabu dhidi ya Barcelona'
Muungana wa waajiri nchini Kenya FKE umesusia sherehe za mwaka huu, na licha ya hayo yote wafanyakazi nchini Kenya wameiambia BBC kuwa wataendelea kuomba dua ili mashauriano kati ya serikali na vyama vya wafanyakazi yazae matunda la sivyo wataendelea kuvumilia na kusalia na mishahara yao ya sasa.
Awali Wafanyakazi wa serikali na makampuni mbali mbali walishiriki maonyesho hayo na muungano wa wafanyakazi nchini Kenya ulituma ujumbe huu kuonyesha baadhi ya wafanyakazi walioshiriki maonyesho.
Tanzania hali si tofauti na Kenya
Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema licha ya kutoa ahadi ya kuongeza mishahara ya wafanyakazi lakini bado anahitaji kujenga uchumi kabla ya kufanya hivyo.
Amesema hatua zinazochukuliwa sasa za kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ni kwa faida ya Tanzania ya leo na kesho.
AFP
Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 1, 2019 katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) mkoani Mbeya katika uwanja wa Sokoine.
"Namshukuru sana Katibu mkuu Tucta...kwa kunikumbusha juu ya ahadi yangu niliyoitoa siku kama ya leo mwaka jana mkoani Iringa lakini niwaambie kuwa muda wangu bado haujaisha,"
Rais Magufuli amewaomba Watanzania waamini kuwa subira yavuta kheri, na akawaomba wasaidie kuujenga uchumi wa taifa lao ili uwe imara kabla ya kupandishiwa mishahara
Amewakumbusha Watanzania kuwa Serikali yake imeongeza ajira za walimu, madaktari na manesi, na akasema ahadi yake ya kutoa ajira bado haijaisha na muda wake wa utawala bado haujaisha."
Amesema miradi iliyoanzishwa itawanufaisha wafanyakazi, wakulima kwa kusafirisha mazao yao, wafugaji, wavuvi lakini inawanufaisha wafanyabiashara wote.
- Wafanyakazi wagoma Afrika kusini
- Wafanyakazi wa nyumbani waandamana Kenya
- Wafanyakazi kulazimishwa wakapumzike Korea Kusini
Comments
Post a Comment