Mvua 'iliyokwama' Tanzania yawasili Kenya ghafla




Mvua yaanza kunyesha nchini Kenya


Hatimaye 'mbingu zimefunguka' nchini Kenya na jiji la Nairobi kwa mara ya kwanza lilipata hali ya unyevu mwaka 2019.
Mvua hiyo iliodaiwa kukwama nchini Tanzania ilinyesha kwa ghafla na kuwapata Wakenya wengi wakiwa hawajajiandaa.
Wachuuzi waliokuwa wakiuza mali yao katika barabara za jiji la Nairobi waliathiriwa na mvua hiyo.
Waendesha magari na raia pia walipatikana wakati ilipokuwa ikinyesha lakini hakuna aliyeonekana akijali.
Wakaazi walionekana wakitembea katika mvua bila kujali kwamba walikuwa wakinyeshewa.
Masaa mawili kabla ya mvua hiyo kunyesha, idara ya hali ya hewa nchini Kenya ilikuwa imetangaza kuwa mvua itanyesha jijini Nairobi, viungani mwake na maeneo mengine.
Raia wengi waliohojiwa walisema kwamba hawakutarajia mvua kunyesha.
''Sikutarajia kwamba itanyesha na nilipokuwa nikiendelea na biashara yangu , mvua ilinyesha na nikalazimika kutafuta hifadhi kwengineko'' , alisema John Kimani ambaye ni mchuuzi.
Wiki iliopita idara ya hali ya hewa kupitia naibu mkurugenzi wake Bernad Chanzu ilikuwa imesema kuwa hakutakuwa na mvua msimu huu.

Comments

Popular posts from this blog

JOB JOB JOB!!!!!!!! Senior Technical Officer - Supply Chain Management

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani.