Kimbunga Kenneth: Waokoaji wahangaika kufikia vijiji vilivyoathiriwa

Kimbunga Kenneth: Waokoaji wahangaika kufikia vijiji vilivyoathiriwa



Kuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi
Image captionKuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi

Wahudumu wa uokozi wanajaribu kufika katika vijiji visivyoweza kufikiwa kwa urahisi ambako kimbunga kikubwa kimesababisha maafa makubwa.
Kuna hofu kuwa maelfu ya watu wamekwama huku mvua kubwa na upepo vikihofiwa kusababisha hatari ya mafuriko na maporomoko zaidi ya ardhi.
Kimbunga Kenneth kipipiga nchi ya Msumbiji tangu siku ya Alhamisi kikiwa na kasi ya kilomita 220 kwa saa , na kimekuja karibu mwezi mmoja baada ya kimbunga Idai kuwauwa watu zaidi ya 900 katika nchi tatu.
Katibu mkuu wa shirika la msaada la kimataifa Amnesty International Kumi Naidoo alisema kuwa vimbunga hivyo viwili ni matokeo ya ,mabadiliko ya tabia nchi kama yalivyotangazwa na wanasayansi walioonya kuwa vimbunga vya aina hiyo vitatokea iwapo wakazi wa dunia wataendelea kuharibu mazingira kupita kiasi ".

Maafisa wanatathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Kenneth kaskazini mwa MsumbijiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaafisa wanatathmini uharibifu uliosababishwa na kimbunga Kenneth kaskazini mwa Msumbiji

" Kuna mambo tusiyoweza kuyakwepa na ukosefu wa haki ambao hatuwezi kuusisitizia vya kutosha ," alisema na kuongeza kuwa : " Watu wa msumbiji wanalipia gharama yya mabadiliko hatari ya tabia nchi wakati hawajafanya lolote la kusababisha tatizo hili ."
Maelfu ya nyumba zimeporomoka, huku mifumo ya umeme ikiharibika na maeneo ya mabonde yamefukumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na droruba.

Baadhi ya familia zilizosambaratishwa na kimbunga Kenneth nchini Msumbiji zikiwa katika makazi ya muda ya msaadaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionFamilia zilizosambaratishwa na kimbunga Kenneth nchini Msumbiji

Mwandishi wa BBC Pumza anasema kuwa uharibifu wa mifumo ya umeme katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Msumbiji umefanya mawasiliano kuwa magumu.
Takribani watu 20,000 wamepelekwa kwenye makazi ya muda ya mahema kwenye vituo vya watu waliosambaratishwa na mafuriko, zikiwemo shule na makanisa, anasema mwandishi wetu.
Kimbunga Kenneth kilikuwa tayari kimewauwa watu watatu katika nchi jirani ya visiwa vya Comoro na walau mtu mmoja ameripotiw akufa nchini Msumbiji baada ya kuangukiwa na mti.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu na lile la Red Crescent Societies yalishirikisha umma uharibifu ulipotokea kupitia mitandao ya kijamii. katika ujumbe huu wa Tweeter , kikundi cha wahudumu wa kujitolea kilionekana na kuthibitisha kuwa kinatoa msaada kw awaathiriwa.
                                                     @R-DJ LYIMO  

Comments

Popular posts from this blog

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

Differences between Gymnosperms and Pteridophytes

Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke