Hoteli ya kifahari yashambuliwa Nairobi


Milipuko na milio ya risasi 14 Riverside, Nairobi, al-Shabab wadai kuhusika




Magari kadha yanawaka moto
Milipuko na milio ya risasi yasikika katika eneo la 14 Riverside, Nairobi kunakopatikana hoteli ya DusitD2.
Milipuko miwili mikubwa ya risasi ilisikika na baadaye ufyatuaji wa risasi.
Watu kadha wamejeruhiwa na wanahudumiwa na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakisaidia na watu wengine wa kujitolea.
Mmoja wa majeruhi amesafirishwa kupelekwa hospitalini.
Maafisa wa polisi wamefika eneo hilo, katika jumba hilo ambalo lina hoteli yakifahari na afisi za kampuni mbalimbali.
Baadhi ya watu waliokwama kwenye vyumba vya jumba hilo wamekuwa wakiandika ujumbe kwenye mitandao wa kijamii wakieleza kwamba wamekwama, au kujificha.

Comments

Popular posts from this blog

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

Differences between Gymnosperms and Pteridophytes

Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke