Paul Kagame afanya mabadiliko makubwa baraza la mawaziri, amuondoa kazini waziri wa ulinzi Rwanda


Paul Kagame afanya mabadiliko makubwa baraza la mawaziri, amuondoa kazini waziri wa ulinzi Rwanda


Rais Paul Kagame akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mataifa yanayozungumza Kifaransa Yerevan mnamo Oktoba 12, 2018Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES

Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri na kumteua Dkt Richard Sezibera kuwa waziri mpya wa mashauri ya nchi za nje.
Jenerali James Kabarebe aliyekuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame amepoteza wadhifa wake kama waziri wa ulinzi na badala yake akateuliwa mshauri wa rais katika masuala ya usalama.
Katika mabadiliko makubwa na ya kushtukiza aliyofanya Rais Kagame wizara 8 kati ya 23 zimepata mawaziri wapya zikiwemo wizara nyeti tatu, wizara ya ulinzi ambayo sasa inaongozwa na Meja jenerali Albert Murasira aliyechukua nafasi ya Jenerali James Kabarebe.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema si wengi walitarajia mabadiliko haya.
Jenerali Kabarebe ambaye amepewa nafasi ya kuwa mshauri maalumu wa rais wa maswala ya ulinzi na jeshi alikuwa mshirika wa karibu sana na Rais Paul Kagame tangu vita vilivyong'oa utawala wa rais Juvenali Habyarimana miaka ya 1990.


Comments

Popular posts from this blog

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

Differences between Gymnosperms and Pteridophytes

Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke