Mwanamume atolewa mswaki tumboni Mombasa, Kenya
HISANI
Madaktari katika Hospitali Kuu ya Mkoa ya Pwani (CPGH) mjini Mombasa, Kenya wamefanikiwa kuutoa mswaki ambao ulikuwa umekwama tumboni mwa mwanamume mmoja kwa siku sita.
David Charo alikuwa akipiga mswaki alipoumeza kimakosa Jumapili wiki iliyopita apokuwa anajiandaa kwenda kazini Bamba, Kilifi.
Kufikia jana, alikuwa ameanza kupata matatizo ya kupumua.
Awali, madaktari walikuwa wamedokeza kwamba angehitaji kufanyiwa upasuaji kuutoa.
Lakini Ijumaa asubuhi, madaktari wakiondozwa na Ramadhan Omar wamefanikiwa kuutoa mswaki huo bila kumfanyia upasuaji wa kawaida.
Badala yake, wamemfanyia upasuaji wa kutumia matundu madogo.
Jumapili, Charo alipokuwa alipoumeza mswaki huo kimakosa, awali ulikwama ndani ya koo kabla ya kutumbukia ndani tumboni.
AFP
Juhudi za nduguye mdogo Julius Charo za kuutoa hazikufanikiwa na ikalazimu wamkimbize hospitali iliyokuwa karibu.
"Tulipompeleka kwenye hospitali hiyo, madaktari walitushauri kumleta katika hospitali hii ya Pwani ambapo alipigwa picha ya x-ray, lakini kwa muda hakufanyiwa matibabu yoyote," Bw Julius aliambia gazeti la Nation.
Comments
Post a Comment