Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke




Familia ya mwanafunzi Akwilina yataka haki itendeke.



Waombelezaji katika msiba wa mwanafunizimarehemu Akwilina, enelo la Mbezi ,jijini Dar es salaam
Image captionWaombelezaji katika msiba wa mwanafunizimarehemu Akwilina, enelo la Mbezi ,jijini Dar es salaam

Maombolezi yanaendelea nyumbani kwa mwanafunzi Akwilina Akwilini anayedaiwa kupigwa risasi na polisi na kufariki baada makabiliano kati yao na wafuasi wa Chadema sikua ya Jumamosi.
Wakizungumza na BBC, ndugu wa marehemu Damian Swai, amesema wanasubiri matokeo ya uchunguzi wa polisi ili waone hatua ambayo itafaa kuchukuliwa.
Damian ameendelea kusema kuwa marehemu alikuwa na ndoto za kusoma na kufaulu na kuwa na maisha yake vizuri lakini, "ndoto yake imekatishwa."
Taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo zilifikia familia kupita Chuo cha Usafirishaji cha NIT ambapo alikuwa anasoma.
Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa hadi Rombo, Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa wazazi wake ambapo ndipo atakapozikwa.
Hata hivyo, serikali kupitia Waziri wa Elimu imesema itagharamia mazishi ya mwanafunzi huyo.

Baadhi ya ndugu ya marehemu walikusanyika kumuomboleza
Image captionBaadhi ya ndugu ya marehemu walikusanyika kumuomboleza

Nae dadake marehemu ameomba "haki itendeke" ili waliohusika na kifo chake wachukuliwe hatua za kisheria.
Hadi sasa polisi 6 wamekamatwa kuhusiana na kifo cha mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Chuo cha usafirishaji Tanzania NITHaki miliki ya pichaPAUL WILLIAM SABUNI
Image captionMarehemu Akwilina Akwilini

Kumekuwa na shinikizo kutoka vyama vya upinzani kama vile chama cha ACT Wazalendo, vijana na Shirika la wanafunzi nchini limemtaka waziri wa maswala ndani nchini humo Mwigulu Nchemba kuchukua jukumu la kisiasa na kujiuzulu kufuatia kisa hicho.

                                          lyimoson@

Comments

Popular posts from this blog

JOB JOB JOB!!!!!!!! Senior Technical Officer - Supply Chain Management

Mwanamume aliyekuwa amebeba cocaine kwenye makalio bandia ashikwa Ureno

wanafunzi 17 kuuawa kwa kupigwa risasi huko Marekani.