Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa DUNIANI
Fahamu nchi zinazotumia bangi kwa kiasi kikubwa Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Nchi nyingi barani Afrika ni kinyume cha sheria kulima, kuuza au kutumia bangi Lesotho Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho. Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini. Zimbabwe kuhalalisha upanzi na matumizi ya bangi Afrika Kusini Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa. Tangu mwezi machi mwaka 2017, ba...